Actions

Chrome ya Moduli

From Joomla! Documentation

Revision as of 16:53, 10 April 2014 by Ayeko (Talk | contribs)

Other languages: català 100% • ‎English 100% • ‎español 100% • ‎français 100% • ‎Bahasa Indonesia 100% • ‎日本語 100% • ‎Nederlands 100% • ‎Kiswahili 100%

Chrome ya moduli inawaruhusu wachoraji wa templeti kuwa na kiwango maalum cha uwezo kwa namna ya pato kutoka kwa moduli litakaloonyeshwa katika templeti zao. Kwa kimsingi, inatoka kwa sehemu ndogo ya HTML iliotayari. Sehemu hii ilioingizwa kabla, baada au mzunguko wa pato kutoka kwa kila moduli, na itaweza kurembeshwa kwa kutumia CSS. Moduli ya chrome inatumika mara nyingi kwa kutoa mizunguko ya mipaka ya moduli, hasa na vipembe vya duara, lakini itaweza kutumika kwa vitu tofauti.

Chrome ya moduli itaamuwa kwa kutumia tabia ya 'style' ndania ya taarifa ambayo inaita moduli. Kwa mfano, taarifa ifuatayo inaweza kutumika katika faili ya index.php ya templeti kwa kuingiza mamoduli katika nafasi ya 'user1' na kuomba moduli ya chrome ya 'custom':

<jdoc:include type="modules" name="user1" style="custom" />

Unaweza kuona kuwa moduli ya chrome hio hio inaomba kwa kila moduli kwa nafasi hio - hii inamaanisha, ukitaka moduli mbili katika safu mmoja, lakini unataka ziwe na chrome tofauti za moduli, nilazima uzitaarishe kama 'nafasi' tofauti (kwa mfano 'user1' na 'user2').

Paketi ya kawaida ya Joomla! 1.5+ ni pamoja na mitindo sita ya difoti ya chrome ya moduli. Kwa vyovyote, nirahisi sana kubadilisha kwa mfumo ya templeti hii inamaanisha kuwa hakuna mipaka kwa mitindo hii - Ni rahisi sana kutengeza mitindo mipya mingi unayotaka!


Angalia pia: Chrome za Kawaida za Moduli