Glossary
From Joomla! Documentation
Glossary ya Joomla! inasaidia kwa kujifunza misemo ya kawaida inayotumika katika mafunzo ya Joomla!, sikirini ya usaidizi na nyaraka ya kina.
Nanga
Nanga imetengezwa kwa kutumia tagi ya <a> HTML. Nanga itakuruhusu kuweka kipendwa ndani ya ukurasa wa HTML. Katika Joomla! unaweza kuweka kipendwa ndani ya makala (kwa mfano kwa kutumia mhariri wa TinyMCE). Hii itakuruhusu kutengeza kiungo ambacho kitakwenda moja kwa moja kwa sehemu hiyo ndani ya makala.
Msimbo wa chanzo cha HTML kwa nanga unaonekana kama yafuatayo:
<a name="nanga_yangu" title="NangaYangu"></a>
Unaweza kuunganisha nanga kutoka kwa ukurasa huohuo kwa kutumia msimbo wa HTML
<a href="#nanga_yangu" ></a>
Ukibofya kiungo hichi, kitakupeleka moja kwa moja kwa sehemu ya tagi ya nanga.
Unaweza kuunganisha nanga katika ukurasa tofauti kwa kuongeza "#" na jina la nanga mwisho wa URL. Katika mfano hapo juu, ikiwa URL wa makala ni http://www.wavutiwangu.com/makala_yangu.html
, alafu unaweza kuunganisha nanga moja kwa moja kwa ukuruasa huu kwa kutumia URL http://www.wavutiwangu.com/makala_yangu.html#nanga_yangu
.
Lahamtindo wa Kuachilia (Cascading Style Sheet, CSS)
Lahamtindo wa kuachia au CSS unatumika kwa kudhibiti onyeso la ukurasa kwa XHTML. Kwa mfano, faili za CSS kila mara zinadhibiti fonti, pembezote, rangi, grapfiki za usuli, na mambo mengineo ya kurasa za wavuti. CSS ziitakuruhusu kutofautisha yaliyomo ya ukurasa wa XHTML kutoka na kuonekana. Katika Joomla!, mafaili ya CSS (kwa mfano, templeti ya.css) kwa kawaida ni sehemu ya templeti.
Angalia pia: Templeti, Suffix ya Darasa la Ukurasa, Suffix ya Darasa la Moduli
Jamii
Kila sehemu ya wavuti wanaoendeshwa na Joomla! au wavuti wa aina yoyote wa CMS unahitaji njia ya kuonyesha na kuhifadhi yaliyomo yake kifikra. Njia ya kawaida ni kwa majamii na majamii ya chini. Joomla! inaruhusu kwa njia nyingi za kuonyesha na kutumia yaliyomo yanayothibitiwa na upangaji kwa jamii. Baadhi ya aina ya yaliyomo ambayo yatapangwa kwa jamii ni Makala (Makuu ya yaliyomo ya kurasa za wavuti), mabana, mawasiliano na viungo vya mitandao.
Uncategorised (ambayo haikupangwa) ni jamii ya difoti iliopeanwa kwa kila aina ya yaliyomo yoyote, ni jamii ya difoti. Jamii Uncategorised si ya kielezo na inapaswa kutumika kwa misingi kama inahitajika kwa ajili ya aina ya yaliyomo ambayo si kuanguka chini ya jamii maalum.
Wakati wa kutengeza na kushirikisha majamii, unapaswa uwe na mpango wa muundo vileunavyotaka. Kama mfano, hii ni njia mojawapo ya jinsi gani utapanga Makala kuhusu ndege. Tengeza majamii mawili ziitwazo "Wanyama" na "Mimea". Chini ya jamii "Wanyama", utaweza kuwa na majamii ya chini ziitwazo "Ndege" na "Mamalia". Chini ya jamii "Ndege", utaweza kuwa na makala tatu kwa majina yake "Mwewe", "Kasuku" na "Shomoro".
- Wanyama
- Ndege
- Mwewe
- Kasuku
- Shomoro
- Mamalia
- Ndege
Unaweza kupanua mfano hapo juu na makala maalum kuhusu fikira tofauti za mwewe, kasuku na shomoro. Anza kwa kutumia "Wanyama" kama jamii ya juu. Weka majamii ya chini "Ndege" na "Mamalia" chini ya jamii ya Wanyama, na pia majamii ya chini "Mwewe", "Kasuku" na "Shomoro" chini ya jamii ya chini "Ndege", kama ilivyoonyeshwa.
Now you can create multiple articles in the Hawk, Parrot and Sparrow sub categories using the different genus or common names of the specific types of these 3 birds.
Majamii yanaundwa kwa kutumia Meneja wa Jamii, ambaye atapatikana katika kusano ya msimamizi (upande wa nyuma) kwa kubofya aina ya menyu ya Yalioyomo, na tena kitu cha menyu cha Meneja wa Jamii kwa aina hii.
Angalia pia: Makala
Chrome
Grafiki ya kusano inayoonekana kwa sifa za maombi wakati mwingine hurejelewa chrome. Angalia Kutumia moduli kidesturi chrome kwa maelezo kuhusu jinsi ya kurekebisha mtazamo wa moduli (kwa maneno mengine, moduli "Chrome").
Komponenti
Prefix ya Jedwali ya Hifadhidata
Prefix ya jedwali ya hifadhidata ni sharti (la herufi chache) zililo ongezwa mbele ya jina la majedwali ya Joomla!. Ukitumia prefix, unaweza kuendesha usasishaji tofauti wa Joomla! kwa hifadhidata moja.
Unaweza kuweka prefix ya jedwali ya hifadhidata wakati wa usasishaji. Pia unaweza kubadilisha baadaye, lakini inahitaji kuingia kwa hifadhidata kwa kutumia maana zaidi ya Joomla, au kiendelezo cha Joomla kama Akeeba Admin Tools, na wavuti wako utakua offline kwa muda fulani.
Waendelezaji wa viendelezo nilazima kutumia sharti #__
kwa kuwakilisha prefix. Hii itabadilishwa na prefix halisi wakati wa Joomla iko offline.
Kiendelezo
Jinda bandia
Orodha ya Kuthibiti Maingizo (ACL)
Kiini
Katika Joomla!, neno "kiini" linalohusiana na mafaili ya kusambazwa yanayotakiwa kwa kutengeza na kusimamia wavuti wanaoendeshwa kwa CMS ya Joomla. Mafaili haya yanaweza kushushwa kutoka kwa wavuti wa Joomla: http://www.joomla.org/download.html. "Kiini" cha Joomla pia uko na jukumu la kimsingi wa kufikia usakinishaji mpya wa Joomla kufanya kazi upesi na urahisi. Ina meneja wa mtumiaji, meneja wa makala, meneja wa miunganisho ya mtandao, meneja wa jamii, meneja wa mawasiliano, na meneja wa menyu. Pia ina meneja wa templeti pamoja na baadhi ya templeti ya kimsingi kwa kuendesha mtazamo wa upande wa mbele (wavuti/mtumiaji), meneja wa moduli pamoja na mamoduli wa kimsingi, meneja wa plugin pamoja na plugin ya kimsingi, na baadhi ya viendelezo "out of the box" kwa kupanua kujumu wa ufungaji wa kimsingi wa Joomla. Viendelezo hivi vya viini havipaswi kuchaganywa na viendelezo ambavyo vinaweza kushushwa kutoka kwa Saraka ya Viendelezo vya Joomla! (Joomla! Extension Directory, JED).
Angalia pia: Joomla Extension Directory.
Lugha
Lugha pengine ni aina za viendelezo vya msingi muhimu na za haki. Lugha zimepangwa kama paketi za ukuu za lugha ama paketi ya lugha ya kiendelezo. Mapaketi haya yanatokana na mafaili ya INI ambayo niyenye majozi ya funguo/thamani. Majozi haya yanapeana utafsiri wa masharti ya maandishi ndani ya msimbo wa chanzo ya Joomla!. Hii itaruhusu ukuu wa Joomla! na komponenti au moduli za mkono wa tatu kuwa za kimataifa. Mapaketi ya lugha ya ukuu pia yatakua faili ya meta ya XML ambayo inaeleza lugha na inapeana maelezo kuhusu fonti kwa kutumia kwa kutengeza yaliyomo ya PDF.
LDAP
Menyu
Mtawala wa Mtazamo wa Modeli (Model View Controller, MVC)
Joomla inashugulika sana na patani ya mchoro wa Mtawala wa Mtazamo wa Modeli.
Ikiwa Joomla inaanza kuandaa maombi kutoka kwa mtumiaji, kama vile GET kwa ukurasa halisi, au POST inayohusiana na data ya fomu, mojawapo ya jambo la kwanza Joomla itakalofanya ni kuchambua URL na kuamua komponeti gani utakuwa na mamlaka ya kupeana maombi, na kupeana uthibiti kwa komponenti hio.
Ikiwa komponenti iliundwa kwa patani ya MVC, itapeana uthibiti kwa mtawala. Mtawala anamamlaka ya kuchambua maombi na kuamua kuwa ni modeli gani unahitaji kudhibitiwa na ombi, na ni mtazamo gani utatumika kwa kuregesha matokeo kwa mtumiaji.
Modeli inajenga gamba kwa data zinazotumiwa na komponenti. Kwa kesi nyingi, data hizi zitatoka kwa hifadhidata - ama hifadhidata ya Joomla au hifadhidata tofauti za nje - lakini modeli pia unaweza kupata data kutoka kwa vyanzo vingine, kama API ya mahuduma ya mitandao yanayoendeshwa katika seva nyingine. Modeli pia unamamlaka ya kusasisha hifadhidata wakati wa mwafaka. Kusudi ya modeli ni kujitenga na mtawala na kuangalia kutoka kwa maelezo na ni vipi data zitapatikana au zitarekebishwa.
Mtazamo una mamlaka wa kutengeza pato ambalo komponenti itatumia kwa kisakuzi. Itatoa witu kwa modeli ya taarifa yoyote inayohitajika, na itapeana fomati ya sahihi. Kwa mfano, mtazamo utaweza kuvuta orodha ya vitu vya data kutoka kwa modeli na kufunga vitu hivyo katika jedwali ya HTML.
Since Joomla is designed to be highly modular, the output from the component is generally only part of the complete web page that the user will ultimately see. Once the view has generated the output, the component hands control back to the Joomla framework which then loads and executes the template. The template combines the output from the component, and any modules that are active on the current page, so that it can be delivered to the browser as a single page.
Kwa kutoa nguvu na urahisi wa ziada kwa wachoraji wa wavuti (ambao wana maslahi ya kutengeza michoro mipya pekee, sio kuchezea msimbo wa msingi) Joomla itagawanya mtazamo wa asili kwa namna mbili: mtazamo wa kando au mpangilio. Mtazamo unaovuta data kutoka kwa modeli (kama patani ya asili ya MVC), lakini tena unapeana data kwa mpagilio, ambao una mamlaka kwa kufomati data na kuwakilisha kwa mtumiaji. Ubora wa ugawanyaji huu ni kuwa mfumo wa templeti wa Joomla unapeana mbinu rahisi kwa kubadilisha mipangilio ndani ya templeti. Haya mabadilisho ya mpangilio (yanajulikana kama "template overrides" kwa sababu ni sehemu ya templeti, hata ikiwa mpangilio (sio templeti) utabadilishwa) yatafungwa pamoja na templeti, na mchoraji wa templeti atapata uthibiti wa ujumla wa pato kutoka kwa kiini cha Joomla na viendelezo vyote vya mkono wa tatu ambavyo vitazingatia na patani ya mchoro wa MVC.
Chrome ya Moduli
Suffix ya Darasa la Moduli
Suffix ya Darasa la Moduli ni paramita katika moduli wa Joomla!. Inwekwa ndani ya skrini ya Moduli: [Hariri] sikirini chini ya Maparamita (Hali ya juu). Kuweka paramita hii itasababisha Joomla! kama itaongeza darasa mpya la CSS au itarekebisha darasa liliopo la CSS kwa elementi ya div
kwa hii moduli maalum.
Wakati Joomla! inazalisha moduli, ni moja kwa moja itatengeza darasa la CSS inaitwa "JedwaliLaModuli" kuweza kuruhusu mtindo wa moduli -- kwa mfano
<div class="JedwaliLaModuli">
Kutengeza darasa jipya, weka paramita ilio na nafasi ya kuongoza. Kwa mfano, maingizo ya nafasi na "DarasaLanguJipya" itatengeza darasa jipya la CSS liitwalo "DarasaLanguJipya ". HTML itabadilishwa kuwa
<div class="JedwaliYaModuli DarasaLanguJipya ">
Kubadilisha jina la darasa liliyoko, weka paramita bila nafasi ya kuongoza. Kwa mfano, maingizo ya "_SuffixYangu" (bila nafasi ya kuongoza) yatabadilisha HTML kwa
<div class="JedwaliYaModuli_SuffixYangu">
Kwa kawaida, unashauriwa kutumia nafasi ya kuongoza kwa kutengeza darasa jipya. Kama hivi, mtindo wa CSS kwa moduli hii ambayo inatumia majina ya kawaida ya madarasa itaendelea kufanya kazi. Unaweza kutumia jina la darasa jipya kwa kuongeza mtindo unaopenda kwa moduli bila ya kutengeza tena msimbo wote wa CSS uliopo. Kumbuka kuwa, ikiwa unatengeza jina la darasa jipya, hakikisha lina jina la kipkee na halina migogoro na majina ya darasa yaliopo.
Angalia Kutumia Suffix za Darasa kwa maelezo zaidi.
Nafasi ya Moduli
Moduli
Suffix ya Darasa la Ukurasa
Suffix ya Darasa la Ukurasa ni paramita katika Vitu vya Menyu wa Joomla!. Inwekwa ndani ya skrini ya Kitu cha Menyu: [Hariri] sikirini chini ya sehemu ya "Maparamita (Hali ya juu)". Hii itasababisha Joomla! kama itaongeza darasa mpya la CSS au itarekebisha darasa liliopo la CSS kwa maelementi ya mpangilio maalum wa Kitu cha Menyu.
Wakati Joomla! inazalisha ukurasa, ni moja kwa moja itatengeza madarasa yaliowekwa awali ya CSS kuweza kuruhusu mtindo wa ukurasa. Kwa mfano, ukurasa inawezakuwa na elementi
<div class="KichwaChaKomponeti">
Kutengeza darasa jipya, weka paramita ilio na nafasi ya kuongoza. Kwa mfano, maingizo ya nafasi na "DarasaLanguJipya" itatengeza darasa jipya la CSS liitwalo "DarasaLanguJipya " na litawekwa kama darasa za maelementi katika hiki Kitu cha Menyu. Kwa kesi hiki, mfano wa hapo juu itabadilishwa kuwa
<div class="KichwaChaKomponenti DarasaLanguJipya ">
Kubadilisha jina la darasa liliyoko, weka paramita bila nafasi ya kuongoza. Kwa mfano, maingizo ya "_SuffixYangu" (bila nafasi ya kuongoza) yatabadilisha HTML kwa
<div class="KichwaChaKomponenti_SuffixYangu">
Kwa kawaida, unashauriwa kutumia nafasi ya kuongoza kwa kutengeza darasa jipya. Kama hivi, mtindo wa CSS kwa komponenti hii ambayo inatumia majina ya kawaida ya madarasa itaendelea kufanya kazi. Unaweza kutumia jina la darasa jipya kwa kuongeza mtindo unaopenda kwa komponenti bila ya kutengeza tena msimbo wote wa CSS uliopo. Kumbuka kuwa, ikiwa unatengeza jina la darasa jipya, hakikisha lina jina la kipkee na halina migogoro na majina ya darasa yaliopo.
Angalia pia: Kutumia Suffix ya Darasa, Kutumia Suffix ya Darasa la Ukurasa katika Msimbo wa Templeti
PHP
PHP ni lugha ya kompyuta ya kuandika maprogramu, imeundwa kwa kutengeza kurasa za nguvu ya mtandao. PHP inatumika kwa mapana na maendelo ya wavuti, na inaweza kupachikwa katika HTML. Kwa kawaida inatumika katika seva ya mtandao; inatuma kodi ya PHP kama ingizo na itatengeza kurasa ya mtandao kama pato. Kwa maelezo zaidi, angalia Wapi nitajifunza kuhusu PHP?
URL Unaofaa kwa Mashini ya Kutafuta (SEF URLs)
URL Unaofaa kwa Mashini ya Kutafuta (SEF URLs) ni neno la kawaida lililo fupishwa kama SEF URL au SEF kiufupi. Kawaida ni URL wa Joomla! utaonekana kama hivi:
http://www.wavutiwako.org/index.php?option=com_content&view=section&id=3&Itemid=41
Unaweza kuhariri na URL na kuonyesha kurasa ya HTML ya tuli kama hivi:
http://www.wavutiwako.org/faq.html
Tangu Joomla! 1.5, kuna mijengo katika uchaguzi kwa kuzalisha SEF URL. Haya yataweza kuwezesha kwa kubadilisha "Matayarisho ya SEO " (Search Engine Optimisation) katika tabi ya upande wa mbele ndani ya sikirini ya Usanidi wa Wakidunia katika upande wa nyuma wa Joomla!. Kuna viendelezo vya mkono watatu ambavyo pia vinatengeza SEF URL wa Joomla!.
Menyu Zinazogawanyika
A split menu is where different levels of a single menu are displayed in two or more locations on a single web page.
Kwa mfano, hitaji ya mara kwa mara ni menyu na vitu vya kiwango cha juu vitakavyoonyeshwa juu ya ukurasa. Ikiwa mtumiaji inabofya katika mojawapo ya vitu, atapelekwa katika ukurasa ambapo menyu ya pili, kwa mfano katika upande wa kushoto wa ukurasa, itaonyesha vitu vya menyu vya kiwango cha pili ndani ya wigo wa kitu cha menyu cha kiwango cha juu.
Menyu zitatokea katika sehemu tofauti za ukurasa, zinahusiana lakini, kwa sababu mojayao inaonyesha vitu vya kiwango cha juu pekee, ambapo nyingine inaonyesha vitu vya kiwango cha pili. Fikra hii inaweza kupanuwa kwa kutia menyu kwa vitu vya kiwango cha tatu na kuendelea.
Hii inaweza tekelezwa kwa Joomla kwa kutumia menyu moja iliyo na viwango vingi, na tena kutengeza moduli za menyu zaida ya moja, na kila moja yao imaanishe kwa kiwango tofauti.
Angalia pia: Menyu
Templeti
Templeti ni aina ya Kiendelezo cha Joomla! kitakacho badilisha njia ya tovuti yako itakavyoonekana. Kuna aina mbili za matempleti zinazotumiwa na Joomla! CMS: Templeti ya Upande wa Mbele na Matempleti ya Upande wa Nyuma. Templeti ya upande wa mbele ni kudhibiti namna ya tovuti yako ni njia gani itawasilishwa kwa mtazamo wa mtumiaji wa yaliyomo kwa wavuti. Templeti ya upande wa nyuma ni kuudhibiti namna ya wavuti wako ni njia gani ya majukumu ya kuitawala kwa kazi iliyotolewa ya usimamizi na Joomla! Msimamizi. Haya yatakuwa ni pamoja na kazi ya kawaida kama vile mtumiaji, menyu, makala, jamii, moduli,componenti plugin na Templeti ya usimamizi.
Angalia pia: Komponenti, Moduli, Plugin
Paketi ya Kuboresha
Katika Joomla! paketi ya kuboresha ni nyaraka ya mafaili ambazo zina mafaili yaliobadilishwa kati ya matoleo ya Joomla!. Ikiwa nyaraka inapakuwa, itabadilisha toleo la zamani la mafaili yaliobadilishwa kwa toleo jipya. Kwa mfano, ikiwa mafaili 50 yamebadilishwa kati ya toleo 1.x.1 na 1.x.2, paketi ya kuboresha kutoka kwa 1.x.1 kwenda kwa 1.x.2 itakuwa na mafaili haya 50. Kabla ya kupakua, itabadilisha mafaili haya 50 na itaboresha toleo lililosakinishwa kutoka kwa 1.x.1 kwenda kwa 1.x.2.
Wakati mwengine mapaketi ya kuboresha yataitwa mafaili ya patch. Kabla ya kusakinisha paketi ya kuboresha, soma makumbuko ya kutolea na Maelekezo ya Kuboresha kuhusiana na paketi ya kuboresha.