Suffix ya Darasa la Ukurasa

From Joomla! Documentation

This page is a translated version of the page Page Class Suffix and the translation is 100% complete.
Other languages:
Bahasa Indonesia • ‎English • ‎Kiswahili • ‎Nederlands • ‎català • ‎español • ‎français • ‎русский • ‎日本語

Suffix ya Darasa la Ukurasa ni paramita katika Vitu vya Menyu wa Joomla!. Inwekwa ndani ya skrini ya Kitu cha Menyu: [Hariri] sikirini chini ya sehemu ya "Maparamita (Hali ya juu)". Hii itasababisha Joomla! kama itaongeza darasa mpya la CSS au itarekebisha darasa liliopo la CSS kwa maelementi ya mpangilio maalum wa Kitu cha Menyu.

Wakati Joomla! inazalisha ukurasa, ni moja kwa moja itatengeza madarasa yaliowekwa awali ya CSS kuweza kuruhusu mtindo wa ukurasa. Kwa mfano, ukurasa inawezakuwa na elementi

<div class="KichwaChaKomponeti">

Kutengeza darasa jipya, weka paramita ilio na nafasi ya kuongoza. Kwa mfano, maingizo ya nafasi na "DarasaLanguJipya" itatengeza darasa jipya la CSS liitwalo "DarasaLanguJipya " na litawekwa kama darasa za maelementi katika hiki Kitu cha Menyu. Kwa kesi hiki, mfano wa hapo juu itabadilishwa kuwa

<div class="KichwaChaKomponenti DarasaLanguJipya ">

Kubadilisha jina la darasa liliyoko, weka paramita bila nafasi ya kuongoza. Kwa mfano, maingizo ya "_SuffixYangu" (bila nafasi ya kuongoza) yatabadilisha HTML kwa

<div class="KichwaChaKomponenti_SuffixYangu">

Kwa kawaida, unashauriwa kutumia nafasi ya kuongoza kwa kutengeza darasa jipya. Kama hivi, mtindo wa CSS kwa komponenti hii ambayo inatumia majina ya kawaida ya madarasa itaendelea kufanya kazi. Unaweza kutumia jina la darasa jipya kwa kuongeza mtindo unaopenda kwa komponenti bila ya kutengeza tena msimbo wote wa CSS uliopo. Kumbuka kuwa, ikiwa unatengeza jina la darasa jipya, hakikisha lina jina la kipkee na halina migogoro na majina ya darasa yaliopo.

Angalia pia: Kutumia Suffix ya Darasa, Kutumia Suffix ya Darasa la Ukurasa katika Msimbo wa Templeti


Namna ya kutumika

Ukiweka suffix ya darasa la ukurasa na nafasi inayoongoza, darasa jipya la CSS litatengezwa. Ikiwa paramita yako haina nafasi inayoongoza, madarasa ya CSS yanayolingana na hii kitu cha menu (kwa mfano "componentheading") yatabadilishwa. Mbinu ya kwanza inatumika mara nyingi, kama kwa kesi hii hautavunja mtindo ulioko wa maelementi ya ukurasa, na utaongeza tu kodi mpya ya CSS kwa mitindo mipya.

Ikiwa hautumii nafasi inayoongeza, itakubidi unakili kodi zote za mtindo wa darasa la Kitu cha Menyu na kudabiri kwa darasa jipya la CSS baada ya kubadilisha CSS.

Unaweza kutumia maparamita ya Suffix ya Darasa la Ukurasa kwa kutengeza madarasa ya kipekee ya CSS ambayo yatakuruhusu kusimba kitu kimoja cha menyu kilichotofauti na chingine.