Chunk

Nanga

From Joomla! Documentation

Revision as of 02:50, 14 April 2014 by Ayeko (talk | contribs)
(diff) ← Older revision | Latest revision (diff) | Newer revision → (diff)

Nanga imetengezwa kwa kutumia tagi ya <a> HTML. Nanga itakuruhusu kuweka kipendwa ndani ya ukurasa wa HTML. Katika Joomla! unaweza kuweka kipendwa ndani ya makala (kwa mfano kwa kutumia mhariri wa TinyMCE). Hii itakuruhusu kutengeza kiungo ambacho kitakwenda moja kwa moja kwa sehemu hiyo ndani ya makala.

Msimbo wa chanzo cha HTML kwa nanga unaonekana kama yafuatayo:

<a name="nanga_yangu" title="NangaYangu"></a>

Unaweza kuunganisha nanga kutoka kwa ukurasa huohuo kwa kutumia msimbo wa HTML

<a href="#nanga_yangu" ></a>

Ukibofya kiungo hichi, kitakupeleka moja kwa moja kwa sehemu ya tagi ya nanga.

Unaweza kuunganisha nanga katika ukurasa tofauti kwa kuongeza "#" na jina la nanga mwisho wa URL. Katika mfano hapo juu, ikiwa URL wa makala ni http://www.wavutiwangu.com/makala_yangu.html, alafu unaweza kuunganisha nanga moja kwa moja kwa ukuruasa huu kwa kutumia URL http://www.wavutiwangu.com/makala_yangu.html#nanga_yangu.

Languages

Other languages:
Bahasa Indonesia • ‎Deutsch • ‎English • ‎Kiswahili • ‎Nederlands • ‎català • ‎dansk • ‎español • ‎français • ‎italiano • ‎svenska • ‎български • ‎русский • ‎العربية • ‎中文(台灣)‎ • ‎日本語